.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 13 Januari 2018

CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAMILIKI WA VIWANDA VYA MAZAO YA MISITU NCHINI KUTATULIWA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu nchini kuwapa ushirikiano wa kutosha pale inapohitajika kwa kuzishughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha wamiliki wa viwanda hivyo hasa wazawa kutoa ajira nyingi kwa wananchi.

Amesema Wizara hiyo haiwezi kufanya kazi pekee yake pasipo kushirikiana na sekta binafsi kwani wao ndo wamiliki wa viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi ambao ndio walinzi wakubwa misitu nchini.

Akizungumza kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, kati ya viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Wawakilishi wa Wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu nchini, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwataka wadau hao wasisite kuwasiliana nae pale wanapokuwa na jambo lolote linalohusu maendeleo ya viwanda vyao

‘’Nimechaguliwa na Mhe. Rais kuja katika Wizara hii kwa ajili ya kufanya kazi nanyi, tufanye kazi kwa ushirikiano’’ alisema Hasunga

Aidha, Naibu Waziri huyo, amelisema Serikali imeanzisha utaratibu wa ugawaji wa vitalu kwa njia mnada na kwa njia ya makubaliano binafsi lengo lake sio kuviua viwanda wa mazao ya misitu vya vinavyomilikiwa wazawa bali ni kutaka kila mwenye sifa asiweze kukosa mgao huo.

Akifafanua kuhusiana na utaratibu huo mpya wa ugawaji wa vitalu ulioanza mwaka jana , Hasunga alisema asilimi 30 ya vitalu imekuwa ikifanyika kwa njia ya mnada na asilimi 70 imekuwa ikifanyika kwa njia ya makubaliano binafsi hali iliyopelekea kupunguza malalamiko na pamoja na vitendo vya rushwa kwa wadau.

‘’Kila mmoja wetu hapa atakuwa shahidi hakuna hata mmoja mwenye kiwanda cha mazao ya misitu aliyekosa mgao kupitia huu utaratibu mpya ulianza kutumika mwaka jana’’

Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu juu ya utaratibu huo mpya ambao wengi ni wazawa kwa kushindwa kushindana na matajiri lakini hata hivyo utaratibu huo kwa njia ya mnada umeisaidia serikali k kupanga bei stahiki ya soko katika njia ya makubaliano binafsi.

Hasunga alisema Serikali ipo tayari kupokea mawazo mapya kutoka kwa wamiliki wa viwanda hivyo kama wataona kuna umuhimu wa kuboresha utaratibu huo mpya wa ugawaji wa vitalu.

Wakati akijibu hoja za wadau hao, Hasunga aliwaagiza waandae ripoti itayoonesha changamoto zinazowakabili na kuiwasilisha ofisini kwake ifikapo tarehe 10 mwezi ujao kwa ajili ya kufanyiwa kazi

Pia, Aliwaagiza wamiliki wa viwandao hao kuunda kitengo kitakachokuwa na jukumu la kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo kujua masoko pamoja na teknolojia rafiki ya kuzalisha bidhaa zao zitakanazo na mazao ya misitu

Awali, Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus wakati akiwasilisha taarifa yake ameiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia wamiliki wazawa viwanda vya mazao ya misitu kwa vile viwanda vilivyo vingi vimeshindwa kujiendesha kutokana na kukosa malighafi kwa kuwa wazao hao wameshindwa kushindana na matajiri wakubwa wakati vitalu vinapouzwa kwa njia ya mnada.

Aliongeza kuwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) iangalie uwezekano wa kupunguza bei za vitalu hivyo kwa kuwa viwanda vingi vimeshindwa kujiendesha kwa vile bei ya soko la mbao limeporomoka kutokana na watu binafsi kuuza mbao kwa bei nafuu zilizotokana na miti iliyovunwa ikiwa michanga.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Wavunaji Sao Hill, Christian Ahiya, ameiomba Wizara kuona uwezekano wa kupunguza tozo 32 zinazotozwa kwa wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu kwa upande wa wilaya Mufundi kwa kuwa hali hiyo imekuwa ukiwaumiza na kuwadidimiza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus (kulia) wakati Rais huyo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus akiwasilisha taarifa ya wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Japhet Hasunga kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kufungua kikao cha wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu mara baada kufungua kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni