.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 15 Januari 2018

LIVERPOOL YATIBUA REKODI YA MANCHESTER CITY YA KUTOFUNGWA EPL

Manchester City imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu baada ya Liverpool kupambana vyema nyumbani na kuibuka na ushindi wa magoli 4-3 katika dimba la Anfield.

Kikosi cha Jurgen Klopp kikicheza mchezo wake wa kwanza bila Philippe Coutinho aliyehamia Barcelona ilistahili ushindi huo uliotibua rekodi ya Manchester City, lakini ukaweka rekodi yao ya kutofungwa katika michezo 18.

Alex-Oxlade Chamberlain aliifungia Liverpool goli la kwanza lakini likaswazishwa na Leroy Sane kabla ya mapumziko, Roberto Firmino akaongeza la pili na kisha Sadio Mane la tatu na Mohamed Salah akafunga la nne.
                                         Mshambuliaji  Sadio Mane akifunga goli al pili la Liverpool
Kocha Jurgen Klopp akipeana mkono na kocha Pep Guardiola baada ya mpira kuisha

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni