SALAAM ZA MWENYEKITI WA BODI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA SIKU YA POSTA AFRIKA 2018
KESHO tarehe 18/01/2018, Shirika letu la Posta litaungana na Mashirika mengine Afrika kuadhimisha kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) mnamo mwaka 1980.
Umoja huu makao makuu yake yapo Arusha Tanzania. Lengo la kuanzishwa Umoja huu ni kusimamia maendeleo ya Posta Afrika.
Pamoja na salaam zangu kwa Katibu Mkuu wa Umoja huu Bwana Younouss Djibrine na watendaji wenzake, napenda kuwapongeza wanaposherehekea miaka 38 ya Umoja huu.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “POSTA: Muundombinu muafaka kwa Serikali katika kufikia Malengo yake ya Maendeleo”.
Kutokana na Posta kuwa na matawi mengi yaliyosambaa katika nchi kuliko watoa huduma wengine hapa nchini, tunapongeza kauli mbiu hii na kwa kweli Shirika limejipanga katika kuhudumia wananchi katika kuwezesha mafanikio yao kibiashara, kama mnavyofahamu mwaka jana 2017 Shirika letu liliibuka kidedea katika kundi la watoa huduma (Trade Facilitation) na kukabidhiwa ngao ya ushindi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli..
Shirika letu limeanza mikakati ya kufungua vituo “Huduma Express” hapa Posta Mpya Dar es salaam na vingine vitaanza Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya na Zanzibar. Katika vituo hivi tunaweza kutoa huduma mbalimbali mahali pamoja “One-Stop-Centre” na hii itasaidia sana Serikali kutoa huduma zake kwa wananchi kwa urahisi zaidi.
Hii inaenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu. “POSTA kama Muundo Mbinu muafaka kwa Serikali katika kufikia malengo yake ya maendeleo”.
Pia Dk. Kondo alitumia fursa hiyo kuelezea kwa muhtasari mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo Shirika lilikabiliana nazo mwaka jana 2017.
Alielezea kuwa Shirika kwa ujumla lilipata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuzindua nembo mpya mwezi Desemba 2017 na sasa liko kwenye maandalizi ya kuboresha muonekano wa Shirika katika ofisi zake nchini kote.
Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya wenye fanaka 2018.
Lt. Col. Mstaafu. Dr. Haruni Kondo
MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni