.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 14 Januari 2018

NAIBU WAZIRI KIJAJI AFANYA UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la Wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha,alisema madhumuni ya baraza hilo ni kuwapa fursa watumishi kupitia wawakilishi wao pamoja na kujadiliana juu ya masuala mbalimbali.(Habari Picha na Pamela Mollel)Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu ArushaMakamu Mweneyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Bw.Juma Kaniki akisoma risala katika uzinduzi huo Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro katika uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)katikati akinyoosha juu mkataba wa kuunda baraza ambao umehakikiwa na kusainiwa na Kamishna wa kazi,wa pili kulia niKaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi,na wakwanza kushoto ni Didas Malekia Mwenyekiti wa tawi la IAA chama kilichounda baraza la wafanyakazi(THTU)
Sehemu ya Baraza la Wafanyakazi Chuo cha Uhasibu Arusha
Baadhi ya wanafunzi chuo cha Uhsibu Arusha wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi kwa umakini ambapo pamoja na mambo mengi Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji aliwasisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa mshiriki mkubwa wa kupambana na rushwa ambayo inajikita katika kupotosha na kumomonyoa maadili.
Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baraza la wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha Tarehe 10 Januari 2018

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni