.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Januari 2018

WANAOISHI MAENEO HATARISHI KUHAMISHWA CHEMBA

SERIKALI wilayani Chemba mkoani Dodoma imesema kuwa imepanga kuwahamisha watu wanaoishi maeneo hatarishi ya kupata mafuriko kutokana zaidi ya kaya 2,000 zimezungukwa na maji katika kata ya Mrijo hadi hivi sasa.

Akiongea wakati akitoa taarifa kwa waratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu waliokwenda kufanya tathimini ya maafa yaliyotokana na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo, mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga alibainisha kuwa mkakati wa muda mrefu walionao ni kuwatafutia wakazi hao maeneo salama.

Odunga Alisema kuwa kwa sasa kamati za maafa zimechukua hatua ya kukabili maafa ya mafuriko kutokana na idadi ya nyumba zilizozungukwa na maji imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo wameanzisha kambi maalum kwa watu ambao nyumba zao zimeanguka kutokana na maafa hayo.

Aliongeza kuwa msaada wa haraka unahitajika kutokana na waathirika hao wa mafuriko kutumia baadhi ya majengo ya madarasa ambayo yanapaswa kutumiwa na wanafunzi ambao wanajiunga na masomo mwaka huu.

“kwa sasa tunahitaji sana mahema, mataulo, mashuka , chakula pamoja na madawa kwajili ya kuwahudumia hawa watu ambao tunao hapa na tukipata vifaa hivyo basi tutaondoka hapa na kwenda kutengeza kambi sehemu nyingine ambayo tumeiandaa maaluum kwajili ya kuwahifadhi hawa watu na kuacha haya madarasa kwajili ya matumizi ya wanafunzi” alisema Odunga.

Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kuwa tayari wilaya imeshaunda kamati mbalimbali ambazo zinahusika katika kusaidia wahanga hao kuwa salama kiafya kwa kuchukua tahadhari zinazoweza kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko.

Naye mratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu Ally Mwatima, alisema kuwa mahitaji yote ambayo yameanishwa na mkuu huyo wa wilaya wameyachukua na watayawasilisha ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema iwezekanavyo.

“Kwanza niwapongeze kwa kukabili maafa kwa mujibuwa sheria,kanuni namiongozo ya menejimentiya maafa, hali hii imesaidia kuokoa maisha ya hawa wenzetu na mahitaji yote mliyobainisha ni ya msingi sana hivyo tutakwenda kuonana pia na kamati ya maafa mkoa ili kuweza kuona na sisi tunaongeza nguvu katika vitu gani vya msingi ambavyo vitawasadia hawa wenzetu”alisema Mwatima.
Mkuu wa wilaya ya Chemba ,Simon Odunga akifafanua jambo wakati kamati ya maafa ya wilaya nakata ya Mrijo walipokutana na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajiliya tahmini ya athari zamaafa ya mafuriko katika katika wilaya hiyo.
Muonekano wa sehemu ya soko wilayani Chemba ambapo ni eneo ambalo wilaya hiyo imepanga kuweka kambi ya waathirika wa maafa ya mafuriko wakati wanapanga mikakati ya kuwapangia makazi salama waathirika hao.
Baadhi ya nyumba ambazo zimezungukwa na maji katika kata ya Mrijo wilayani Chemba kutokana na maafa ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyenya wilayani humo.
Baadhi ya waathirika wa maafa ya mafuriko wakiwa katika kambi ya muda iliyo andaliwa na kamati ya maafaya wilaya ya Chemba kutokana na thari za maafa ya mafuriko wilayani humo.
Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (shati jeupe), Eward Boniphace, akifuatilia majadiliano wakati kamati ya maafa ya wilaya na kata ya Mrijo walipokutana na wataalamu kutoka Ofisi hiyo kwa ajili ya tahmini ya athari za maafa ya mafuriko wilayani Chemba mkoani Dodoma.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni