.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Januari 2018

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA SERENGETI NA BUNDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengti, Bw. William Mwakileme kutokana na mchango mkubwa wa hifadhi hiyo katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Robada wilayani Serengeti. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 19, 2017. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Hunyari baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati hiyo wilayani Bunda Januari 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mashine za kusukuma maji wakati alipoembelea mradi wa chanzo cha maji Bunda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ushirika wa Igembe Sabo wilayani Bunda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfereji wa maji wakati alipozindua chama cha ushirika cha Igembe Sabo kinachojishughulisha na kilimo cha mpunga wilayani Bunda Januari 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwakabidhi hati ya usajili wa chama viongozi wa chama cha ushirika cha Igembe Sabo cha Bunda , Malongo Mashimo ambaye ni Katibu (kulia) na Maria Nengwa ambaye ni Mwenyekiti wa Ujenzi baada ya kuzindua ushirika huo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 19, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni