.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 13 Februari 2018

ATAKAYEMPATIA MWANAFUNZI MIMBA KUKIONA CHA MOTO

          MKUU wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Mhandisi Mtemi Saimon

                                                                                      Na Shushu Joel,Kwimba.

MKUU wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Mhandisi Mtemi Saimon ametangaza hali ya hatari kwa wanaume wenye tabia ya kuwakatisha masomo wanafunzi wa kike kwa kuwapachika ujauzito na kupelekea kuwakatisha masomo yao.

Rai hiyo ameitoa jana alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya hiyo katika kujadili maendeleo ya wilaya yake katika Nyanja mbalimbali pamoja na kutatua changamoto za wananchi dhidi ya watumishi wa serikali.

Akuzungumza na wakuu wa idara,viongozi wa dini,wafanyabiashara,watu mashuuli na wazee aliwahitaji kwenye kikao hicho cha kujadili maendeleo ya kwimba,hivyo aliwataka watu hao kupanga ni jinsi gani wazazi na serikali wakishirikiana watatokomeza changamoto ya mimba kwa watoto wao.

Aliongeza kuwa kwa wazazi wenye tama na kuoata mali kupitia watoto wa kike sasa hivi si kipindi chake kwani watu kama hao watachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yao ya kuwakatisha wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo katika maisha yao,

“Tumekubaliana mambo manne ya kuzingatia katika kikao chetu na wadau wangu,kumlinda mtoto wa kike,kumsomesha mtoto wa kike,kuwakemea wote wenye nia ya kuwaozesha watoto wa kike kwa lengo la kujipatia mifugo na la mwisho kushirikiana katika kuwafikisha wale wote wanaonekana kuwanyemelea watoto wa kike” Alisema Mtemi.

Kwa upande wake meneja wa shirika la mapato wilaya humo Mihayo Mitili amewakumbusha wananchi na viongozi kuwa mstali wa mbele katika ulipaji wa kodi ya majengo kwa lengo la kuisaidia serikali ya awamu ya tano yenye lengo la kuwasaidia wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali katika wilaya yetu.

Aliongeza kuwa juhudi zinazofanywa na mkuu wa wilaya ni za msingi na zinapaswa kuungwa mkono na kila mwananchi wa kwimba mwenye machungu na elimu ya kumwendeleza mtoto wa kike katika kufanikisha malengo yake ya baadae kupitia elimu.

Naye bshehe mkuu wea wilaya hiyo ya kwimba Rajabu Hassani amemtaka mkuu wa wilaya kutokuteteleka katika juhudi zake za ufanikishaji wa maendeleo kwani tangu aanze kazi katika wilaya yetu watu wengi wamekuwa wakifanya kazi na kuacha kushinda kwenye vijiwe kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Aidha alisema kuwa viongozi wa dini zote tuko tayari kufunga hata siku kadhaa kwa ajili ya maombi maalumu kwa ajili ya taifa letu jinsi linavyopambana katika ufanikishaji wake wa maendeleo kwa wananchi wake wanyonge ili waweze kunufaika na raslimali zao zilizoko nchini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni