Timu ya Bayern Munich imeichakaza
Besiktas iliyokuwa na wachezaji 10 kwa kupata ushindi mnono wa magoli
5-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16.
Wenyeji wameshinda mchezo wao wa 14
mfululizo baada ya kuutawala mchezo huo katika kipindi cha pili dhidi
ya Besiktas ambayo mchezaji wao Domagoj Vida alipewa kadi nyekundu.
Katika mchezo huo Thomas Muller
alifunga magoli mawili naye Kingsley Coman akafunga goli moja huku
mfungaji anayeongoza kwa magoli Robert Lewandowski akifunga mawili.
Thomas Muller akifunga goli kati ya magoli yake mawili aliyofunga jana
Mchezaji Kingsley Coman akifunga goli la pili la Bayern Munich
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni