Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola amegoma kumlaumu Raheem Sterling kwa kuchangia kuinyima
ushindi City dhidi ya Burnley baada ya mchezaji huyo kupoteza nafasi
nzuri ya kufunga.
Manchester City ikiwa inaongoza kwa
goli 1-0 zikiwa zimebakia dakika 20 mchezo kumalizika, Sterling
alishindwa kuongeza goli la pili katika umbali wa yadi sita baada ya
kukutana na krosi ya Kyle Walker.
Kitendo hicho kilimfanya azomewe na
mashabiki wa timu yake na kisha kulazimika Sterling kutolewa nje
kupumzika na baadaye Johann Berg Gudmundsson alipoisawazishia Burnley
zikiwa zimebakia dakika nane mpira kuisha.
Mchezaji Raheem Starling akipoteza kizembe nafasi nzuri ya kuongeza goli la pili
Mchezaji Johann Berg Gudmundsson akishangilia baada ya kuisawazishia Burnley
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni