.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 20 Februari 2018

DAWASA NA DAWASCO ZATAKIWA KUPELEKA HUDUMA ZA MAJI PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR

NaibuWaziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso (wa pili toka kulia) akiwa na
katibu tawala wa Wilaya ya Temeke, Edward Mpogolo wakati wakipatiwa
maelezo machache juu ya uharibifu wa miundo mbinu ya maji inayofanywa na
wananchi wasio waaminifu wakati wa ziara ya Naibu huyo aliyoifanya
katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kujionea miradi mbali mbali ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso akiangalia moja ya mradi wa maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amezitaka mamlaka
zinazohusika na usambazaji wa huduma ya maji safi na taka (DAWASA na
DAWASCO) kuendelea kusambaza huduma pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Kauli hiyo ameitoa Februari 19, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara
yake aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kuweza kujionea
miradi mbali mbali iliyoanzishwa ili kuweza kuwafikia huduma ya maji kwa
urahisi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni