Na Mahmoud Ahmad Chemba
Halmashauri ya wilaya ya Chemba imekadiria katika mpango wa fedha za bajeti yake kwa mwaka 2017/18 jumla billion 32.3 kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupokea mpango wa Fedha wa mapato na matumizi ya halmashauri zikiwa kama nakisi ya bajeti ya Halmashauri hiyo
Akisoma Taarifa ya mpango wa mapendekezo ya Bajeti ya mwaka 2017/18 mkuruigenzi wa Halmashauri hiyo Semistatus Husein Mashimba amesema kuwa pamoja na mapato na matumizi ya Halmashauri inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukubwa wa eneo na ukosefu wa usafiri wa ufikaji katika shughuli za kila siku hivyo kutofikia lengo. La makusanyo yake na umaliziaji wa miradi kwa kasi.
Amesema kuwa bajeti iliyopita wameitekeleza kwa asilimia 64% ambapo ya mwaka huu wa fedha hadi kufikia robo ya pili wameitekeleza kwa 16% ikiwa ni bajeti ya mapato ya ndani ambapo ametanabaisha kuwepo kwa changamoto mbali mbali zinazoifanya halmashauri hiyo kushindwa kufikia lengo ikiwemo uchelewaji wa fedha kutoka serikali kuu,ukosefu wa usafiri hususani magari huku halmashauri hiyo ikiwa na Km za mraba 7653.
Wananchi kuwa na Ari ndogo ya uchangiaji wa mapato ya ndani kunakosababisha kutofikia malengo ya maendeleo na mapato ambapo amemshukuru mh. Rais dkta John Magufuli kutekeleza bajeti yao ya watumishi ikiwemo mishahara yote kwa asilimia 100 na fedha zote za miradi ya maendeleo kwa mwaka huu 2017.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rajabu Omary akitoa hutoba wakati wa kufungua kikao hicho amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kuwahasisha wananchi kuweza kuchangia mapato ya ndani ya halmashauri hiyo kwani kimeshindwa kukidhi miradi ya maendeleo na kushindwa kumalizika kwa wakati na hivyo kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya ndani.
Amesema kuwa wajibu wao ni kutekeleza majukumu yao bila kusukumwa na mtu na ndio msingi uwajibikaji katika eneo lako la kazi na si kusukumwa na mtu huko ndio kunashindwa kuipeleka mbale halmashauri yetu ambayo bado ni change na inahitaji watu sahihi wa kuendeleza kwa moyo na uzalendo
Amesema kuwa pamoja na ukosefu wa usafiri wa kufika katika maeneo mengi ya wilaya hiyo bado mpango wa kuibua vyanzo vya ndani vya halmashauri hiyo itasaidia kuweza kufikia malengo ya bajeti yao ya halmashauri naona kama kutakuwa na ufuatiliaji hii itasaidia kufanikisha malengo ya bajeti yetu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni