.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 14 Februari 2018

HALMASHAURI YA LONGIDO YAPEWA GARI LA CHANJO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Stephen Kiruswa gari aina Tunland Double cabin kwa ajili ya kuboresha huduma za chanjo na afya katika jimbo hilo.

Amemkabidhi gari hilo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo, Bw. Jumaa Mhina na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Longido, Bw. Sabore ole Moloimet.

Waziri Mkuu amesema amekabidhi gari hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa alipofanya ziara wilayani Longidi, Agosti, 2017. Gari la kutolea huduma za chanjo lilikuwa ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinaikabili wilaya hiyo.

Kwa upande wake, Dkt. Kiruswa alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido. “Gari hili ni zuri sana na linahimili mazingira ya wilaya ya Longido.”

“Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma mbalimbali wilayani Longido zikiwemo za afya na maji licha ya jimbo hilo kukaa muda mrefu bila ya kuwa na mbunge.”

Amesema atahakikisha gari hilo linatunzwa na linatumika kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa ambayo ni huduma za chanjo na afya pamoja na huduma za mama na mtoto.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 14, 2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni