Romelu Lukaku amefunga mara mbili
wakati Manchester United ikiifunga Huddersfield kwa magoli 2-0 na
kutinga robo fainali ya kombe la FA.
Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji
alifunga goli la kwanza katika dakika ya tatu tu ya mchezo, akiuwahi
mpira wa kupenyezewa na Juan Mata.
Lukaku alifunga goli lake la 21
katika msimu huu katika kipindi cha pili baada ya kuwatoka kasi
mabeki wa Huddersfield na kuwahi pasi ya Alexis Sanchez.
Romelu Lukaku akimpoteza mahesabu kipa Jonas Lossl na kupachika goli la kwanza
Romelu Lukaku tena akiachia shuti na kufunga goli la pili katika mchezo huo wa Kombe la FA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni