Mudumu wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kulia, akiwahudumia wanakijiji wa Kirando, Wilayani Nkasi katika
Madawati ya dharura Mkoani Rukwa Februari 8, 2018
NA MWANDISHI WETU, NKASI
WAKAZI wa Mkoa wa Rukwa wamesema mpango wa Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO), kufungua madawati ya Kuhudumia na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zitolewazo na Shirika hilo umekuwa na faida kubwa.
Madawati ya dharura Mkoani Rukwa Februari 8, 2018
NA MWANDISHI WETU, NKASI
WAKAZI wa Mkoa wa Rukwa wamesema mpango wa Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO), kufungua madawati ya Kuhudumia na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zitolewazo na Shirika hilo umekuwa na faida kubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mahojiano yaliyofanyika kwenye
baadhi ya maeneo ya Mkoa huo, wakazi hao wamesema, hivi sasa wanauwezo wakupata huduma kwa haraka na kujua masuala mbalimbali yahusuyo umeme na hata wanapohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme kwenye majumba yao imekuwa rahisi kwani wanaelewa ni hatua gani za kufuata ili kupatiwa huduma hiyo muhimu katika maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Uongozi wa TANESCO Mkoa wa Rukwa umefungua jumla ya madawati matano ya kusikiliza na kutoa elimu kwa wananchi katika wilaya za Sumbawanga mjini, Nkasi na Laela, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Herini Mhina amesema Februari 8, 2018.
Katika mahojiano, mkazi wa Kirando, Bi. Veronica Ndenje alisema kupitia
madawati hayo yamewawezesha kupata huduma kwa haraka kwani kabla ya utaratibu huo iliwabidi wasafiri umbali mrefu kupata huduma za TANESCO.
“Madawati hayo yamesaidia kupunguza gharama kwani zamani ilibidi kutumia nauli kuafata huduma wilayani na kupoteza muda mwingi kufuata huduma.” Alisema.
Kupitia madawati hayo wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali za
TANESCO kama vile huduma ya kujua namna gani wanaweza kuunganishiwa umeme kwa mara ya kwanza, huduma za dharura pia kupata elimu mbalimbali zinazohusu umeme na shughuli za TANESCO.
Naye mkazi mwingine Bw. Mohmmedi Waziri toka Kalambo alisema madawati
haya yamesaidia wananchi kuachana na vishoka na matapeli kwani kipindi cha nyuma kabla ya madawati vishoka ambao hujitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa TANESCO kitu ambacho sio kweli walikuwa wakiwatapeli wananchi kwa kuwaahidi wangewasaidia kupatiwa huduma za umeme kwa haraka.
Madawati hayo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani alilolitoa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani humo, Mhandisi Mhina, Waziri Dkt. Kalemani aliuagiza uongoizi wa Shirika hilo Mkoani Rukwa kusogeza ofisi zake karibu na wananchi kupitia madawati ya huduma kwa wateja.
“Madawati haya sio tu yamesaidia kuwasogezea karibu huduma wananchi bali
pia yameongeza makusanyo ya fedha zitokanazo na huduma mbalimbali na ikiwa ni pamoja na kutokomeza tatizo la vishoka wanaojifanya ni wafanyakazi wa TANESCO”. Alisema Mhanidsi Mhina.
Aidha Mhandisi Mhina alisema, Shirika lina mpango wa kuongeza madawati
kutoka matano hadi kumi na sita ili kupanua mtandao wa huduma kwa wananchi, katika awamu ya REA awamu ya Tatu ya kuwafikishia umeme wananchi vijijini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni