Na Shushu Joel
BARABARA ni msingi mkubwa katika nchi kwa ajili ya kupiga hatua ya maendeleo katika mataifa mbalimbali,kila nchi inahitaji kuwa na barabara nzuri ili kufanikisha katika hadha yake ya kufanya shughuli zote za usafirishaji wa haraka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingie pasipo kuwepo na kikwazo cha aina yeyote ile.
Katika barabara nyingi kuna alama nyingi zinazonyesha ishara ya kitu fulani kwa lengo la kuwasaidia waendeshaji wa vyombo vya moto kama vile magari,pikipiki,baiskeli na vingine vingi ambavyo vinatumia barabara kama njia ya usafirishaji.
Alama za barabarani ziko nyingi na zote zikiwa na maana zake na zinatakiwa kufuatwa ili kuzuia ajali,kuna alama za pundamilia ambazo huonyesha kuwa mwenye chombo cha moto anatakiwa kusimamisha gari lake ili watembeao kwa miguu kuweza kupita bila usumbufu wa aina yeyote ile.
Lakini kwa madereva walio wengi wanashindwa kufuata sheria za barabarani kwa kisingizio cha kupoteza muda,hivyo hawasimami kwenye pundamilia ili kuwafanya watu watembeao kwa miguu waweze kuvuka kwa urahisi kama vile taratibu zilivyowekwa na serikali ili kuwasaidia watu wasio na vyombo vya moto pia ikiwemo watu wenye ulemavu kuvuka kwa urahisi.
Alama za pundamilia zimekuwa zikipuuzwa sana na vyombo vya moto pasipo na sababu yeyote ile ingawa madereva wote wanaijua sheria hiyo inataka wafanye nini punde wanapofika katika barabara na kukuta kuna alama za pundamilia(Zebra).
Joseph Moshi ni mkazi wa kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu anasema kuwa pundamilia ama sehemu zile ambazo utumika kuvuka kwa watembea kwa miguu zimekuwa na changamoto nyingi kutokana na watumiaji wengi wa vyombo vya moto kutokutia sheria za barabarani.
Anasema kuwa madereva wengi ambao hutumia Barabara wamekuwa wakaidi wakubwa kwa kutokusimama kwenye pundamilia ili watembea kwa miguu waweze kupita pasipo kutapa kwa buguza juu ya hofu ya kugongwa na magari kwa watembeaji hao.
Anaeleza kuwa kibaya zaidi hadi wanafunzi wa shule mbalimbali nao wamekuwakumbwa na changamoto ya kusubili kupungua kwa magari yaishe ama yapungue ndio waweze kuvuka kwa urahisi ili waweze kuelekea kwenye vituo vya daladala au majumbukani kwao.
“Serikali ya awamu ya tano inaombwa kulitolea macho jambo hili kwani ni hatari kwa usalama wa watembea kwa miguu ili waweze kunufaika na uwepo wa vivuko hivyuo yaani pundamilia “Alisema Masanja Shigongo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari kishamapanda iliyoko mkoani Simiyu anasema kuwa inawachukua muda kuweza kufanikiwa kuvuka barabara pindi wakiwa wanaenda shuleni hii ni kutokana na mara nyingi asubuhi madereva wanakuwa na haraka sana ya kusafirisha abiria wanoenda makazini.
Anasema kuwa wanapokuwa wamefika penye kituo cha kuvukia kwa sasa wanamkuta askari wa usalama barabarani ambaye inawarahisishia sana wao kuweza kuvuka na kuweza kwenda kuingia madarasani kwani madereva humwogopa askari huyo kwa kuogopo kupigwa faini ya kutokuzingatia sheria ya kusimama kwenye kivuko ili watembea kwa miguu waweze kuvuka.
“Tukiwa tunatoka shuleni mara nyingi tunasaidiwa na mlinzi wa shule ambaye hutangulia kwenye pundamilia na kuzisimamisha gari zinazotoka mjini na zile zinazokwenda mjini na kisha wanafunzi kupata fursa ya kuvuka barabara kwa urahisi” Alisema mwanafunzi huyo.
Naye David Benard ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Kiloleli iliyoko Mkoa wa Simiyu na ni mwanafunzi wa darasa la pili anasema wanafunzi wa kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu ndio wanapata changamoto nyingi za uvukaji wa barabara kutokana na umri wao kuwa ni wa chini kwa kuogopa magari.
Anasema wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la pili hutoka darasani kwa makundi makundi mpaka barabarani hivyo kama kunakuwa hakuna trafiki pale barabara basi hali yao huwa mbaya katika uvukaji wa barabara pale kwenye pundamilia ingawa ni haki yao kisheria kuvuka kwanza.
Hivyo anawaomba madereva wote nchini kuzingatia sheria za vivuko ili wanaotakiwa kuvuka katika vivuko hivyo waweze kupita kwa usalama wa hali ya juu.
Seleman Tekele ni dereva wa gari dogo lenye namba T 222 CVT gari aina ya Toyota Wish na hufanya shughuli za taxi kwenye wilaya ya Busega na Magu anasema kuwa madereva wengi hatuzingatii sheria za barabani na ndio maana tumekuwa ni shida katika taifa hili.
Tekele anasema kuwa ili kutokomeza kabisa ajali za barabarani ni vyema kukawa na faini za vifungo kwa madereva ambao wanakuwa hawapendi kuzingatia sheria mpaka pale wanaposhurutishwa kwa faini au kifungo,hivyo hali ya namna hii ni changamoto kubwa kwa serikali yetu kwa watu kama hawa.
Endapo madereva wasiozingatia sheria ya kuheshimu pundamilia ama vivuko vya watembea kwa miguu wanakamatwa basi iwe ni mifano kwa madereva wengine wenye tabia za kutokuzingatia sheria.
“Tunaiomba serikali kuweka mkazo katika barabara ya Mwanza-Musoma kwani walio na magari makubwa (Mabasi) wamekuwa na tabia ya kutokupunguza mwendo kwenye alama ya aina yeyote ile kwa kisingizia cha kutokuwepo kwa trafiki kwenye maeneo hayo” Alisema
Naye Pamba Sarehe ni miongoni mwa madereva wa magari ya abilia aina ya Tata yenye namba T 842 CZH ambaye hufanye safari zake kutoka Bariadi kwenda Mwanza anasema ni kweli madereva ni wachache sana wanaozingatia sheria za vivuko vya pundamilia hii ni kutokana na hata watembeaji wa miguu wenyewe kutokuwa na mazoea ya kuvuka kwenye vivuko hivyo.
Anasema kuwa ili sheria hii iweze kuzingatiwa ni sisi madereva kutambua umuhimu wa watembea kwa miguu pale tunapowaona wakiwa wanahitaji kuvuka au kusimama hata kama hakuna mtu ambaye anahitaji kuvuka katika maeneo ya pundamilia labda tunaweza kufanikiwa kwa kasi.
Muhammad Shaban almaruufu kama Aluta ni mwanaharakati wa usalama barabarani kutokea taasisi isiyo ya kiserikali ya Asasi ya wazalendo na maendeleo Tanzania (AWAMATA) ambayo inaelimisha kuhusu Usalama Barabarani,Angani,Majini na Relini kupitia jina SALAMA SALMINI anasema kuwa vivuko vya watembea kwa miguu vimekuwa havizingatiwi si kwa madereva wala watembeaji wa miguu ambao ndio wahusika wakuu wa vivuko hivyo kutokana na wote kutokujua sheria zipi ni sahihi juu ya vivuko hivyo vinatakiwa vitumikaje kwao wavukaji na madereva.
Anasema kuwa ni muhimu sana kwa watembea wa miguu kuzingatia kuwa sehemu salama kwao katika kuvuka barabara ni pahali ambapo pana kivuko cha pundamilia ilio karibu ili waweze kuvuka katika hali ya usalama.
“Katika nchi zingine serikali huwachukulia hatua kali watembea kwa miguu kwa kuwatoza faini iwapo watavuka katika sehemu zingine tofauti na pale palipo na pundamilia,mara nyingi hali hii hufanyika kwa fundisho kwa watembea wa miguu kutambua wajibu wao wa kuzingatia sheria za barabarani”Alisema Aluta.
Akaeleza kwamba Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari.
Kwahiyo, dereva anapaswa kupunguza mwendo na kusimama kuruhusu watembea kwa miguu wavuke na hatakiwi kuwasha double hazard kwani hiyo inamaana gari linashida.
Aluta ameliomba jeshi la polisi nchini kupambana na madereva wanaovunja sheria za barabarani kwa kutokuzingatia wala kuziheshimu alama za barabarani ili iweze kuwa funzo kwa madereva wengine walio na akili kama hizo hasa wasiosimama wakiona watu wanataka kuvuka na dereva hasimami.
Vivuko vya barabarani viko vingi sana nchini na vina maana kubwa kwa watembea kwa miguu cha msingi ni madereva wetu kuweza kuvizingatia bila shuruti ili na watembea kwa miguu wapate fursa ya kuvuka bila buguza pindi wafikapo kwenye maeneo ya pundamilia.
Anasema kuwa kupitia asasi yao wameandika barua kwa Naibu Waziri ili kumuomba Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kuweza kuwa na namba za simu kama vile ilivyo kwa mamlaka nyinge kama Takukuru na Zima Moto ili iwe vyepesi kwa watu kuweza kuwapatia taarifa za kiusalama barabarani
Kwa upande wake kamanda wa usalama barabarani nchini ASP Fortunatus Muslim anasema kuwa sheria ziko wazi na madereva wote wanajua sema wanachokifanya ni kutokuzingatia tu sheria za barabarani kwa makusudi hivyo jeshi la polisi limejipanga kwa hili ili kuweza kuwapeleka mahakamani au kuwatoza faini madereva ambao watakaobainika kukaidi alama hizo.
Anasema kuwa kifungu cha 65 kipo wazi na kinajieleza kabisa juu ya madereva kuweza kuzingatia sheria za vivuko na kwa yule atayekaidi sheria hiyo basi mahakmani panamuhusu.
Anasema kuwa changamoto si kwa madreva tu bali hata watembea kwa miguu bado na wenyewe wanamatatizo
Kwa kujichukulia sheria za kuvuka mahali popote pale hata kama hakuna pundamilia hali inayopelekea kuwepo kwa kero kwa upande wa madereva katika kusimamisha magari yao ili watu hao waweze kuvuka huku hakuna ishara ya aina yeyote ile juu ya kuvuka kwa binadamu.
Amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwapatia elimu watoto ili waweze kujua ni namna gani wanapaswa kuvuka barabara pindi wanapokuwa wanahitaji kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wao,hivyo wazazi kwakushirikiana na jeshi la polisi watafanikiwa kwa urahisi na si kuliachia jeshi la polisi tu katika masuala ya ulimishaji wa matumizi ya barabara.
Baadhi ya changamoto ni pamoja na Watembea kwa miguu kuvuka popote hata kama kuna kivuko karibu, baadhi ya sehemu kutokuwa na vivuko, kufutika kwa alama za pundamilia lakini kubwa ni baadhi ya madereva kutopunguza mwendo na kusimama kuruhusu watembea kwa miguu wavuke salama hivyo ili tunazidi kulisimamaia kwa ukaribu ili kusitokee ajali hata moja kwenye vivuko vya watembea kwa miguu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni