Philippe Coutinho amefunga goli lake
la kwanza akiwa na Barcelona na kuisaidia timu yake kuibuka na
ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Valencia na kutinga fainali ya Copa del Rey.
Coutinho, akicheza kwa mara ya tano
tangu uhamisho wa paundi milioni 142 akitoka Liverpool aliingia
katika kipindi cha pili na kufunga goli kufuatia krosi ya Luis
Suarez.
Barcelona ambao ni mabingwa mara
tatu mfululizo wa Copa del Rey ilipata goli lake la pili kupitia kwa
Ivan Rakitic.
Lionel Messi akimpongeza Philippe Coutinho baada ya kufunga goli
Luis Suarez akipambana na kipa Jeume Domenech wa Valencia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni