Timu ya Leicester City imeweka kando
sakata la uhamisho wa Riyad Mahrez baada ya mchezaji huyo raia wa
Algeria kuisaidia kutinga robo fainali ya Kombe la FA, kocha wa timu
hiyo Claude Puel amesema.
Mahrez, ambaye alirejea kikosini
baada ya kukosekana mazoezini kwa siku 10, baada ya pendekezo la
kuhamia Manchester City kugonga mwamba, alimtengenezea nafasi ya
kufunga mshambuliaji Jamie Vardy na kufanya matokeo kuwa 1-0 dhidi ya
Sheffield United.
Mpira uliopigwa na Jamie Vardy ukitinga wavuni na kuandika goli pekee katika mchezo huo
Jamie Vardy akifunga goli ambalo hata hivyo lilikataliwa na refa msadizi katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni