Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki (wa pili) wakiangalia ramani ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kinachotarajiwa kujengwa na Hospitali ya Hubert Kairuki hivi karibuni Bunju jijini Dar es Salaam.Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG
Serikali imetoa pongeza kwa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki kupitia Hospitali ya Hubert Kairuki kwa kujipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ali Hapi kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.
"Hatua Moja nzuri sana kwa manispaa yetu, maana huduma hii itapatikana hapa nchini jambo ambalo linaleta faraja sana kwa kuboresha huduma za afya kwa vile awali huduma kama hizo zilikuwa zikipatikana nje ya bara la Afrika... Mungu ni mwema itapatikana Tanzania," alisema Dkt. Dugange.
Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki alisema kuwa tatizo hilo lipo dunia nzima, na shirika la afya duniani lilitoa takwimu milioni 48 wanachangamoto ya kupata watoto. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki akielezea juu ya ujenzi wa kituo hicho cha kisasa.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kujionea shughuli mbali mbali zilizokuwa zikiendeshwa na Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) kwa kipindi chote tokea Febriari 1-6, 2018 katika kuadhimisha Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone, Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki pamoja na mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange.
Mpiga picha wa Gazeti la Nipashe, Mpochi akipatiwa huduma. Mwandishi na mpiga picha wa Kajunason/MMG akipatiwa huduma.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni