Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mathew Mtigumwe (mwenye miwani) akitoa ufafanuzi namna ambavyo serikali imeanza kusambaza dawa za pamba kwa wakulima, baada ya kupokea malalamiko ya uhaba wa dawa, kushoto ni mkulima wa Pamba Tindigwe Masuke alipotembelewa shambani kwake mkoani simiyu. (PICHA ZOTE NA SHUSHU JOEL)
Na Shushu Joel,, Simiyu.
SERIKALI imewahakikishia wakulima wa Pamba Mkoani Simiyu kuwapatia pembejeo za kilimo ili kukabiliana na wadudu waharibifu ambao wameanza kushambulia zao hilo.
Hayo yalibainishwa juzi na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe alipofanya ziara ya kukagua mashamba ya wakulima na kujionea changamoto zinazowakabili, ikiwemo mazao yao kushambuliwa na wadudu katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Alisema kuwa, awali mkoa wa simiyu kupitia bodi ya pamba, walikuwa wamepanga kusambaza chupa milioni 1.8 kwa wakulima, lakini baada ya kuona hamasa ya wakulima imekuwa mkubwa, wameongeza na kufikia chupa milioni 2.
‘’tumeanza kusambaza pembejeo kwa wakulima mkoani Simiyu baada ya kuona mahitaji ya dawa ni makubwa…awali tulipanga kusambaza chupa milioni 1.8, Lakini mahitaji yamekuwa ni makubwa tumeongeza na kufikia chupa milioni 2 ili kusuru zao hilo’’ alisisitiza Katibu Mkuu.
Aliongeza kuwa wizara ya kilimo imesambaza watalamu 30 nchini ili kusaidiana na wataalamu kilimo ngazi ya mkoa, wilaya na kata katika kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya dawa, pia namna ya kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao.
Mtigumwe aliwataka wataalamu wa kilimo kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ili kuhakikisha dawa zinazosambazwa zinatumika ipasavyo.
‘’maafisa ugani saidieni wakulima kuhakikisha dawa zinatumika ipasavyo na siyo kupelekwa kwenye mahindi, lakini pia wakulima waelimishwe juu ya vipimo wakati wa kupulizia, kulingana na maelekezo ya dawa’’ alisema Mtigumwe.
Tindigwe Masuke mkulima wa Pamba kijiji cha Mbiti alisema kuwa dawa zinazosambazwa na serikali hazitoshelezi mahitaji ya wakulima ambao wahamasika kulima, wamekuwa wakipata kidogokidogo hali inayowafanya kushindwa kuwakabili wadudu wa pamba.
‘’tangu nianze kulima kisasa nimeona mafanikio, lakini changamoto kubwa ni upatikanaji wa dawa, kama dawa zitafika kwa wakati, tunatarajia kuongeza mavuno kwa sababu pamba ni nyingi sana mwaka huu’’ alisema Salu Omera Mkulima wa pamba Kijiji cha budalabujiga.
Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya Pamba kanda ya Ziwa, Jones Bwahama alisema kuwa serikali kwa kusirikiana na bodi ya Pamba imeleta timu ya wataalamu saba katika mkoa wa simiyu ili kusaidia na maafisa ugani kuelimisha wakulima jinsi ya matumizi sahihi ya pembejeo.
Mkoa wa Simiyu unahitaji chupa za dawa 1,810,839 huku kukiwa na jumla ya wakulima wa pamba 309,511 ambao wamelima ekari 602,409 likitarajiwa kuzalisha tani 421,686.3 za pamba kwa wastani wa kilo 700 kwa ekari moja.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni