.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 27 Februari 2018

SPORTPESA KUKARABATI NYUMBA YA MADAKTARI ZANZIBAR

Pichaya pamoja kati ya (Baadhi ya wawakilishi/Uongozi wa SportPesa Tanzania) na uongozi wa Kizimkazi mkunguni mara baada ya kuzindua na kukabidhiwa mradi wa kujenga nyumba ya madaktari pichani, Kizimkazi Mkunguni, mkoa wa kusini, Zanzibar. Nyumba hizo zinatarajiwa kuchukua takribani miezi sita mpaka kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa uongozi wa Kizimkazi.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas akiweka saini kwenye kitambu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kizimkazi, Mkunguni.

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri nchini ya SportPesa Limited, imekubali kufanya  ukarabati wa nyumba kwa ajili ya madaktari wawili wa Kituo cha Afya,  Mkunguni eneo la Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Akizungumza wakati wa  ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti kutoka SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema:
“Ikiwa bado tuko mwanzoni mwa mwaka 2018, kampuni yetu tumeamua kutoa mchango  wetu kwa jamii ya Zanzibar kwa kumalizia ujenzi wa nyumba ya madaktari  ambayo ujenzi wa awali ulifanyika miaka 30 iliyopita, ujenzi mpya ni  pamoja na kuongeza vyumba ili nyumba hiyo iweze kukaliwa na madaktari
wengi zaidi.

Kwa Wanazanzibari wote, sisi kama SportPesa tupo kwa ajili yenu na si kwa
upande wa Bara tu na ndiyo maana tumeamua kukarabati makazi ya madaktari kwani wapo kwa ajili ya kuokoa maisha yetu na ya watu
wanaotuzunguka.

Ujenzi wa nyumba hizi itaanza haraka iwezekanavyo na  itachukua si zaidi ya kipindi cha miezi sita hadi kukamilika.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa nyumba hiyo, Diwani wa Wadiyamuyuni, Mustafa  Mohammed Haji alianza kwa kuwakaribisha wawakilishi kutoka SportPesa  kwenye wilaya yake na Zanzibar.

“Napenda kuipongeza kampuni yenu  kwa kazi nzuri mnayoifanya ikiwa pamoja na mambo mbalimbali mnayofanya  ili kuendeleza na kukuza sekta ya michezo nchini.

Nilipopata taarifa juu ya ujio wenu kiukweli nilifarijika sana maana nawaamini na  nategemea mambo mazuri kutoka kwenu kwani kwa maraya kwanza kusikia  SportPesa ni kipindi kile mlivyoichukua timu yetu ya Jang’ombe kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup mwakaj ana.”

Huu utakuwa ni  muendelezo wa huduma za kijamii ambazo kampuni ya SportPesa imeendelea  kuchangia ili kubadili maisha ya Watanzania katika Nyanja mbalimbali za  kimaisha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni