Tottenham iliyotanguliwa kufungwa
imepambana kiume na kulazimisha sare ya magoli 2-2 dhidi ya Juventus
katika mchezo wao wa kwanza wa kuwania kutinga hatua 16 bora ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Jijini Turin.
Kikosi hicho cha Tottenham
kinachonolewa na Mauricio Pochettino kilikuwa nyuma kwa magoli 2-0
ndani ya dakika 10 baada ya Gonzalo Higuain kufunga goli la kwanza
dakika ya pili na kisha kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika
ya tisa.
Harry Kane alikuwa wa kwanza
kuchomoa goli la kwanza baada ya kumzunguka kipa Gianluigi Buffon
kufuatia pasi ya Deli Alli, kisha Higuain akakosa penati. Spur
ilipata goli lake la pili kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Christian
Eriksen.
Mshambuliaji nyota wa Tottenham Muingereza Harry Kane akifunga goli baada ya kumzunguka kipa
Gonzalo Higuain akifunga goli la pili la Juventus kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni