Refa aliyelenga kumkata buti
mchezaji na kisha kumtoa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa soka
nchini Ufaransa amefungiwa kuchezesha soka kwa miezi sita.
Refa huyo Tony Chapron alilala chini
na kumkata buti kwa makusudi mchezaji wa timu ya Nantes, Diego
Carlos wakati wa mchezo wa ligi mwezi uliopita.
Refa Chapron, 45, alimpiga buti
mchezaji huyo aliyekuwa ameshampa kadi ya njano awali, na kisha
akampa kadi ya pili ya njano.
Refa Tony Chapron akimkata buti mchezaji Diego
Carlos wa Nates
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni