Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema marehemu Swai alikuwa hakubali kushindwa kwa kuhakikisha anatatua tatizo linalohusiana na mabomba ya maji kwa wakati wote anapokuwa kazini.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Bi. Hanna Kibopile alisema marehemu ameacha pengo kubwa kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.
Naye meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, Bw. Daimon Mwakyosa alisema marehemu alikuwa akifanyakazi kwa bidii na hakukubali kushindwa.
“Marehemu alikuwa akiijua vyema kazi yake na hakukubali kushindwa nakumbuka wakati nikiwa JNIA na tukiwa tumepangwa shift (zamu) moja hakuna kilichoshindikana kwake kuhusu fani yake aliijua vyema kazi yake,” alisema Bw. Mwakosya.
Bi. Fatma Matimba, Kaimu Meneja Utawala JNIA, alisema marehemu Swai alikuwa mchapakazi, ambapo mwaka jana alichaguliwa kuwa mfanyakazi hodari. Pia aliwahi kupewa cheti cha ufanyakazi hodari mwaka 2001 kinachotolewa TUGHE.
Marehemu Swai alizaliwa mwaka 1960 wilaya ya Rombo, na kupata elimu katika shule ya msingi Kilesi mwaka 1976, na baadaye kujiunga na Chuo cha Ufundi cha Makalema akisomea fani ya ufundi bomba daraja la tatu, na baadaye kujiendeleza katika Chuo cha Ufundi cha Chang’ombe mwaka 1988 na VETA mwaka 2007.
Marehemu aliajiriwa na TAA mwaka 1984 akiwa kama fundi bomba daraja la tatu na baadaye alijiendeleza na kufanikiwa kusoma hadi kufikia daraja la kwanza. Marehemu ameacha mjane Bi. Honoratha Emmilian ambaye naye ni mfanyakazi wa TAA katika Idara ya Utawala akiwa kama mhudumu.
Marehemu Jerome Swai
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (kulia), akimpa pole Bi. Honoratha Emmilian aliyefiwa na mume wake marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba (JNIA), alifariki tarehe 26 Februari, 2018 kwenye hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni