.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Februari 2018

WAZIRI MKUU KUZINDUA MPANGO MKAKATI WA AFYA MOJA NA DAWATI LA URATIBU WA AFYA MOJA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, tarehe 13 Februari, 2018 katika ukumbi wa Karimjee Hall Jijini Dar es Salaam, atazindua Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Uratibu wa Afya Moja. 

Mpango Mkakati wa Afya Moja (2015-2020) unalenga kuimarisha mfumo waAfya moja nchini, kwa kuimarisha juhudi na ushirikiano uliokuwepo wa sekta mbalimbali katika kuzuia, kujiandaa na kukabili magonjwa yanayoambukiza kwa kujumuisha sekta za Afya ya Binadamu, Wanyama (Wanyama pori na Mifugo) na Mazingira. 

Dawati la Uratibu wa Afya moja ambalo limeanzishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu , chini ya Idara ya Kuratibu Maafa, litaratibu shughuli za afya moja kama ilivyo Afya moja ni Dhana inayojumuisha Sekta ya Afya ya Binadamu, Wanyama (Wanyama pori na Mifugo) na Mazingira ili ziweze kushirikiana kwa pamoja katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri Binadamu. 

Tafiti mbalimbali duniani zinaonesha kuwa asilimia 60% ya vimelea vya magonjwa vinatoka kwa wanyama hususan wanyama pori na baadae kusababisha magonjwa kwa binadamu Katika kuboresha Afya ya Binadamu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Sekta zote za Afya nchini (Afya ya Binadamu, Wanyama (pori na Mifugo) na Mazingira, imeandaa uzinduzi wa Mpango na Dawati hilo ili kuweza kuimarisha ushirikiano baina ya sekta hizo. 

Aidha Wananchi wanaombwa kushiriki ili kuweza kuelewa vyema dhana ya Afya moja kwani kutakuwepo na maonesho katika viwanja vya Karimjee ambapo wataalum wa Afya moja watakuwepo wakionesha shughuli wanazozifanya katika kutekeleza AFYA MOJA. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI , OFISI YA WAZIRI MKUU, 12 Februari,2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni