Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe leo amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Bi Sarah Cooke na kufanya mazungumzo ofisini kwake, Makao Makuu ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, mjini Dodoma kwa ajili ya kujadili changamoto katika sekta ya Maji.
Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa kuangalia jinsi serikali ya Uingereza inavyoweza kusaidia kuwezeshwa kujengwa kwa bwawa la Falkwa, nia ikiwa ni kutatua changamoto ya maji katika mji wa Dodoma ambao unatarajiwa kuwa na wakazi wengi kulinganisha na hapo awali.
Waziri ameiomba serikali ya Uingereza kusaidia ujenzi huo kutokana na umuhimu wake katika mji wa Dodoma ikizingatiwa kuwa Makao Makuu ya Serikali yamehamia hapa hivyo mahitaji ya huduma ya maji kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
Aidha, Mhandisi Kamwele ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania kwa misaada mbalimbali inayotolewa kupitia Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (Department for International Development - DFID) katika kusaidia sekta ya Maji kupitia mfumo wa malipo kulingana na matokeo (Payment by Results).
Katika mazungumzo hayo ilibainika kuwa matumizi ya fedha katika Halmashauri nchini kupitia mfumo huo, matumizi ya fedha yamekuwa ni madogo kulinganisha na lengo lililokusudiwa. Hivyo Waziri amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliagiaji, Profesa Kitila Mkumbo kushirikiana na DFID kubaini changamoto na kuzitatua haraka iwezekanavyo.
Balozi amemuomba Waziri wa Maji kutatua changamoto zinazojitokeza ili kuweza kufanikisha malengo yaliyowekwa baina ya Serikali zao na kumuahidi Waziri Kamwele ushirikiano wa dhati katika kuinua sekta ya maji nchini ambapo mpaka sasa Serikali ya Uingereza imeshachangia kiasi cha Pauni milioni 750 kusaidia jitihada mbalimbali za serikali za kuleta maendeleo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni