Ni Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mkoani
Manyara,DK.Mary Nagu (wa kwanza kutoka kushoto) akimpongeza aliyekuwa
diwani wa Kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda mara baada ya kutangaza
azma yake ya kujiunga na CCM.
Ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Manyara,Simon Lulu akipokea kadi ya Chama Cha ACT Wazalebdo kutoka
kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda.
Ni Aliyekuwa diwani wa kata ya
Gihandu kwa tiketi ya ACT Wazalendo, MATHAYO SEMUHENDA akipokea kadi
ya CCM baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
Ni Aliyekuwa diwani wa kata ya
Gihandu,Mathayo Semuhenda akila kiapo cha uadilifu mara baada ya
kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi(CCM).
Na Jumbe Ismaily
ALIYEKUWA diwani wa kata ya
Gihandu,wilayani Hanang,Mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama cha ACT
Wazalendo,Mathayo Samuhenda amejiuzulu udiwani wa kata hiyo na
kujiunga na Chama Chama Mapinduzi (CCM).
Akitangaza azma yake hiyo ya
kujiuzulu katika nafasi yake ya udiwani wa kata hiyo kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Gihandu,Samuhenda alisisitiza kwamba aliamua kujiuzulu na kuwaacha
wapiga kura wake siyo kwa njia ya ukatili bali alifikia maamuzi hayo
kwa lengo la kuwaunganisha wananchi wote wa kata hiyo.
Aidha alifafanua kwamba katika
kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa wananchi wa kata hiyo wana
matatizo ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kutokana na
wanasiasa kutumia mtaji huo kuomba kura.
“Inatosha wanasiasa sisi tutumie
shida ya maji ili tuoate kura tuondoke,inatosha..na watu wa Gihandu
nawaomba sana hiyo ikiletwa kama sehemu ya mnada mzuri tu wa mtu
kujinadi mkataeni inatosha tumeumia vya kutosha.”alisisitiza
Samuhenda.
Hata hivyo diwani huyo aliyejiuzulu
aliweka bayana kwamba umefika wakati sasa kwa wanasiasa kubadili
ajenda za kupatia kura za Gihandu na isiwe upatikanaji wa huduma ya
maji safi na salama kwani hiyo sasa imekuwa ni kejeli.
Akimpokea diwani huyo,Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu alikemea tabia ya baadhi ya viongozi
wa kisiasa wanaoendeleza makundi licha ya kuwa hivi sasa siyo wakati
wa kumpeni na badala yake aliwataka kuvunja makundi hayo na
kusisitiza juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo
yao.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo
alisisitiza pia kwamba suala la kuvunja makundi siyo la hiyari bali
ni la lazima kutokana na makundi hayo baadhi ya wanachama mchana
wanakuwa CCM huku usiku wanatumikia Vyama vya upinzani.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Hanang,Methew Darema alimpongeza diwani huyo kwa kitendo chake cha
ujasiri cha kujiuzulu nafasi aliyokuwa nayo pamoja na kwamba ni hivi
karibuni alitembelewa na kiongozi wake wa kitaifa kwa lengo la
kuhamasisha watu kujiunga na chama hicho.
Kwa upande wake baadhi ya wananchi
wa Kijiji cha Gihandu,Stephano Ngudu alisema mwaka 2008 kila
mwananchi alichangia shilingi 86,500/= kwa ajili ya ujenzi wa shule
ya sekondari na Hosteli mbili,lakini mpaka leo hakuna ujenzi wowote
wa majengo hayo uliokamilika na fedha walizochanga hawajarudishiwa.
MWISHO.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni