Kocha wa Chelsea Antonio Conte
anahisi kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Barcelona kilichoitoa timu
yake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hakikuwa cha “haki”.
Magoli mawili kutoka kwa Lionel
Messi pamoja na mmoja kutoka kwa Ousmane Dembele likiwa goli lake la
kwanza akiwa na Barcelona yalitosha kufanya matokeo ya jumla kuwa
4-1.
Kipigo hicho kimeathiri nafasi ya
Chelsea kucheza michuano hiyo msimu ujao, ambapo sasa itabidi
wapigane kumaliza ligi Kuu ya Uingereza katika nafasi nne za juu.
Lionel Messi akifunga goli lake la kanza ndani ya dakika tatu tu ya mchezo
Ousmane Dembele akifunga goli la pili la Barcelona likiwa ni goli lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo
Kocha wa Chelsea Antonio Conte akimpongeza Lionel Messi kwa kumkumbatia baada ya kumalizika mechi




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni