.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Machi 2018

BALOZI SEIF AELEKEA CUBA KWA ZIARA MAALUM

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka Kushoto akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya China ya ZTE Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Kampuni ya ZTE Kanda ya Mashariki ya Katina Afrika Bwana Darren Zhao kati kati akisisitiza jambo wakati ujumbe wake ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
  Balozi Seif Rais wa Kampuni ya ZTE Kanda yaMashariki ya Kati na Afrika Bwana Darren Zhao akimkabidhi Balozi Seif zawadi Maalum kutoka kwa Uongozi wa Kampuni yake ya ZTE.
Balozi Seif akimkabidhi Bwana Darren Zhao zawadi ya Mlango wa Zanzibar kama ishara ya kuifungulia mlango zaidi wa uwekezaji Kampuni ya ZTE Visiwani Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar leo mchana kupitia Mjini Dar es salaam kuelekea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum.


Katika ziara hiyo Balozi Seif ameondoka Nchini akifuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya wasaidizi wake.

Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Kisauni Zanzibar Balozi Seif aliagwa na baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu wa SMZ, Watendaji wa Serikali pamoja na Viongozi wa Vyama vya Kisiasa viliopo hapa Nchini.

Ziara ya Balozi Seif Nchini Jamuhuri ya Cuba pamoja na mambo mengine
atapata fursa ya kuwatembelea baadhi ya Madaktari Wazalendo wa 
Zanzibar wanaoendelea kupata Mafunzo yao ya ngazi ya juu ya Shahada ya Uzamili ya Udaktari.

Madaktari hao Wanane wa Awamu ya kwanza ni kati ya wale 15 walioteuliwa kupata mafunzo ya juu Nchini Cuba ikiwa ni miongoni mwa waliomaliza mafunzo yao kupitia Mpango Maalum wa masomo ulioasisiwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Cuba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ziara hiyo Maalum ya Balozi Seif imelenga kuendeleza ushirikiano wa Kihistoria wa muda mrefu uliopo kati ya Jamuhuri ya Cuba pamoja na Zanzibar hasa katika Sekta ya Afya ambayo zimeleta mafungamano ya Nchi hizo rafiki Kisiasa na Utamaduni.

Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alikutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao
wa Mawasiliano ya ZTE wenye Makao Mkuu yake Nchini Jamuhuri ya Watu wa
China ulioongozwa na Rais wake Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika.

Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliishukuru na kuipongeza Kamuni ya ZTE kwa kufanikisha uwekaji wa Mkonga wa Taifa Awamu ya Kwanza kazi ambayo imekamilika Mnamo Mwaka 2012 kazi ambao itakuwa kichocheo muhimu katika kuimarisha sekta ya huduma za Uchumi na kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

Akizungumzia awamu ya Pili ya uwekaji wa Mkonga wa Taifa ambao umeelekea zaidi katika huduma za Kijamii na Kiserikali kupitia mfumo wa Mtandao wa Kisasa E- Government, E – Health na E – Tax alisema mabadiliko makubwa yameanza yameanza kupatikana.

Balozi Seif alisema mashine za Kisasa tayari zimeshafungwa ikiwemo MRI na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi katika Sekta ya Afya ambapo kabla
walilazimika kuzifuata huduma hizo nje ya Zanzibar na kutumia gharama
kubwa.

Kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa Mapato kwa njia ya mtandao ambapo ZTE
inaendelea na mazungumzo yake na Bodi ya Mapato Zanzibar Balozi Seif alisema angependa kuona Mfumo huo { E – Tax } unafanya kazi Zanzibar
ili Serikali ijitosheleze kimapato.

Alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba Mfumo huo wa E – Tax unapotumika
vizuri mapato ya Taifa huongezaeka kutokana na kudhitiwa vyema ukusanyaji wake sambamba na maisha ya Wananchi wake kutengemaa.

Naye kwa upande wake Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya ZTE Bwana Darren Zhao alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ZTE imeongeza uwezo wa Kitaalamukatika kuona huduma wanazotoa zinakwenda na kasi ya KiduniaKimtandao.

Bwana Darren aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wake uliyoiwezesha Kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma zake Tanzania na Zanzibar jkwa ujumla.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
08/03/2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni