Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA Ndugu Gianni Infantino amemshukuru Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia kwa kazi nzuri ya maandalizi ya mkutano wa FIFA wa maendeleo ya mpira (FIFA Football Executive Summit) uliofanyika Februari 22, 2018 Dar es Salaam,Tanzania.
Infantino amesifia mapokezi na maandalizi yaliyofanywa na TFF katika mkutano huo mkubwa uliofanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.
Katika barua yake aliyomuandikia Rais wa TFF Ndugu Karia ,Infantino amesema wameondoka na kumbukumbu zisizosahaulika kuhusu Tanzania ikiwemo urafiki uliojengeka wakati wote waliokuwepo Tanzania.
Aidha Infantino ameshukuru kwa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwenye mgahawa wa Cape Town Fish Market lakini pia kwa kukutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Kassim Majaliwa.
Ameshukuru ukarimu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla huku pia akimshukuru binafsi Waziri Mkuu Ndugu Kassim Majaliwa
Amesema FIFA kwa pamoja wameridhishwa na maandalizi na shughuli zote za mkutano huo na wamepokea mrejesho chanya kutoka kwa wajumbe wote waliohudhuria.
Infantino pia amepeleka salamu za shukrani kwa mjumbe wa kamati ya utendaji CAF Ndugu Leodger Tenga,Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Ndugu Kidao Wilfred na timu yake kwa ukarimu waliouonesha na kujitolea kulikofanikisha mkutano huo.
Katika hatua nyingine Infantino ameridhishwa na utendaji kazi wa TFF tokea Ndugu Karia ameingia madarakani pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Kidao akiwataka kuendelea kusimamia mpira katika utaratibu stahiki wenye uwazi kama wanavyofanya sasa.
Tayari msafara wa FIFA umerejea Zurich yalipo Makao Makuu ya Shirikisho hilo.
DROO KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUFANYIKA LEO
Droo ya Kombe la Shirikisho la Azam inafanyika leo Ijumaa Machi 2, 2018 saa 5 asubuhi Makao Makuu ya Azam Tv wadhamini wa mashindano hayo.
Droo hiyo itahusisha timu nane(8) zilizofanikiwa kufuzu hatua hiyo ya Nane bora.
Timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Young Africans na Azam FC za Dar es Salaam,Singida United ya Singida,Njombe Mji ya Njombe,Mtibwa Sugar ya Morogoro,Tanzania Prisons ya Mbeya,Stand United ya Shinyanga na JKT Tanzania ya Dar es Salaam.
SIMBA NA STAND KUCHEZA UWANJA WA TAIFA LEO
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa 19 inaendelea leo kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya Shinyanga
Mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Mwamuzi wa katikati Florentina Zabron kutokea Dodoma ,Mwamuzi msaidizi namba moja Ferdinand Chacha wa Mwanza,mwamuzi msaidizi namba mbili Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza,mwamuzi wa akiba Gelmina Simon wa Dar es Salaam na kamishna wa mechi anatoka Arusha,Peter Temu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni