Sehemu ya Ndege ambao ni kivutio kimojawapo kikubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambao hutegemea pia uwepo wa Maji katika maeneo hayo ambayo kwa sasa yameanza kukauka kutokana na Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na Binadamu .
Mkuruenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi (Mwenye kofia) akiwaonesha Makatibu Wakuu waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara maeneo ya Ziwa Manyara ambayo yameanza kukauka.
Eneo moja wapo la Vivutio vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara likionekana kuanza kukauka kutokana na Athari za kimazingira zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu zikiwemo ,Kilimo Uchimbaji wa Madini katika maene ya jirani na Ziwa hilo.
Vibanda vinavyotumiwa na Wachimbaji wa Madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Moja ya Mtambo unaotumika katika shughuli za Uchimbaji wa madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ukiwa umehifadhiwa katika eneo mojawapo la Uchimbaji.
Maeneo ambayo shughuli za Uchimbaji wa Madini umekuwa ukifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Kijana akifanya shughuli ya uchekechaji wa Mchanga katika moja ya mito inayo peleka maji Ziwa Manyara ,shughuli hi imekuwa ikifanyika kwa lengo la kujipatia Madini ana ya Dhahabu ,Hata hivyo zoezi hili linatajwa kuwa moja ya Uharibifu wa Mazingira unaochangia kukauka kwa Ziwa Manyara.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akiwanesha baadhi ya Makatibu Wakuu namna ambavyo athari za kimazingira zimeanza kuonekana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakitizama kwa mbali Ziwa Manyara.
Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wa serikali katika mikoa ya Arusha na Manyara mara baada ya kihitimisha ziara hiyo. Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni