Mzunguko wa 22 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaendelea wikiendi hii Machi 11, 2018 kwa kuchezwa mechi tano (5)
Mechi mbili za mzunguko huo zilizokuwa zichezwe Machi 11, 2018 zimebadilishiwa tarehe.
Simba waliokuwa wacheze ugenini dhidi ya Njombe Mji mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya Simba kuomba kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata muda wa maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.
Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mchezo wao dhidi ya Young Africans unaochezwa leo Machi 9, 2018.
Mechi nyingine za mzunguko wa 22 zitakazochezwa Jumapili Machi 11, 2018
AzamFC vs Mbao FC (Azam Complex,Chamazi)
Ruvu Shooting vs Mbeya City (Mabatini)
Singida United vs Ndanda (Namfua)
Majimaji vs Lipuli (Majimaji)
Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar (Sokoine)
YOUNG AFRICANS VS TOWNSHIP ROLLERS YAINGIZA MILIONI 56,245,000
Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Young Africans ya Tanzania na Township Rollers ya Botswana uliochezwa Jumanne Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni Hamsini na Sita laki mbili na elfu arobaini na tano(56,245,000).
Mchezo huo uliingiza mashabiki Elfu Tisa Mia Tisa Sitini na Moja(9,961) .
VIP A waliingia Watazamaji Tisini na Tisa(99) kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 1,980,000,VIP B na C waliingia Watazamaji 991 kwa kiingilio cha shilingi 10,000 ikapatikana jumla ya shilingi 9,910,000,majukwa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 8,871 kwa kiingilio ncha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 44,355,000
Mgawanyo wa mapato
VAT 8,579,745.76
Selcom 3,318,455.00
TFF 2,217,339.96
Uwanja 6,652,019.89
Young Africans 28,825,419.50
Gharama za mchezo 3,991,211.93
BMT 443,467.99
CAF 2,217,339.96
SIMBA VS AL MASRY WAINGIZA MILIONI 85,045,000
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa uliozikutanisha Simba ya Tanzania na Al Masry ya Misri uliochezwa Jumatano Machi 7,2018 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni Themanini na Tano Elfu Arobaini na Tano(85,045,000).
Mchezo huo uliingiza mashabiki Elfu Kumi na Nne Mia Saba Tisini na Nane(14,798).
VIP A waliingia Watazamaji 250 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000,VIP B na C waliingia Watazamaji 557 kwa kiingilio cha shilingi 15,000 ikapatikana jumla ya shilingi 8,355,000,majukwa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 13,644 kwa kiingilio ncha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 68,220,000
Mgawanyo wa mapato
VAT 12,972,966.10
Selcom 5,017,655.00
TFF 3,352,718.94
Uwanja 10,058,156.83
Simba 43,585,346.28
Gharama za mchezo 6,034,894.10
BMT 670,543.79
CAF 3,352,718.94
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni