Arsenal imeweka kando matatizo yake
ya hivi karibuni ya kiwango duni cha soka na kufanikiwa kuiengua AC
Milan katika ligi ya Europa kwa magoli 2-0.
Washika mitutu hao wa London
walitinga katika dimba la San Siro wakiwa na rekodi ya kufungwa
michezo minne mfululizo na kuhatarisha kibarua cha kocha Arsene
Wenger.
Henrikh Mkhitaryan alikuwa wa kwanza
kufunga goli ambalo ni goli lake la kwanza tangu kuhamia Arsenal na
kisha Aaron Ramsey akafunga goli la pili.
Henrikh Mkhitaryan akiifungia Arsenal goli la kwanza katika mchezo huo
Aaron Ramsey akifunga goli la pili baada ya kunasa krosi ya Mesut Ozil
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni