Na Mwandishi Wetu
KITUO cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kitaendelea kutoa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na ofisi zote zinazofanya shughuli zake kwenye kiwanja hicho.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Juma Yange wakati wa kufunga mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika kwa washiriki kupata nadharia na baadaye vitendo yaliyofanyika kiwanja hicho.
Afande Yange amesema kwa kuwa wafanyakazi wengi hawajui namna ya kujiokoa wakati wa majanga ya moto, hivyo wanafanya mafunzo hayo kuwa endelevu kwa kuyafanya kuwa endelevu, endapo moto utatokea waweze kujiokoa na kuokoa mali.
“Mafunzo haya yana madhumuni ya kuwawez moto kwenye sehemu yake ya kazi, kufahamu vyanzo na vitu vinavyosababisha moto na vifaa vya huduma vya kwanza vya kuzimia moto vilivyopo eneo lake la kazi, hivyo litakuwa endelevu,” amesema.
Kwa upande wake, Bi. Julieth Fonga wa Kampuni ya General Aviation Services inayofanya kazi zake katika jengo la Kwanza la abiria (TBI) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ameomba mafunzo hayo kutolewa mara kwa mara ili kuwaweka tayari kwa janga hilo la moto.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sajini Maria Gulam amesema wananchi wawe makini na moto, ambao unatokana na muunganiko wa kemikali unaofanywa na vitu vitatu kwa uwiano maalum, ambavyo ni joto, hewa safi na kiwashio.
Sajini Gulam amesema wananchi watambue kuwa moto upo katika madaraja manne ambayo ni ‘A’ yenye viwashio vya asili kama majani, kuni, mkaa, karatasi; daraja ‘B’ inaviwashio vya asili ya kimiminika kama mafuta taa, petrol, diseli, mafuta ya kula; huku daraja ‘C’ ni asili ya gesi na ‘D’ inatokana na michemko ya madini na hutokea zaidi kwenyte viwanda vya kutengeneza mabati, mitambo ya vipuri.
Hata hivyo, Sajini Gulam amesema mafunzo haya ya zimamoto na uokoaji yanatolewa kwa taasisi za umma na binafsi kwa gharama nafuu, ili waweze kujua namna ya kujiokoa na kupiga simu namba 114 ya kuomba msaada wa gari la zimamoto.
Kamishna Msaidizi wa Zimamoto, Hamis Telemkeni (mbele) akitoa maelezo kwa washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuzima moto yaliyofanyika kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo. KITUO cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kitaendelea kutoa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na ofisi zote zinazofanya shughuli zake kwenye kiwanja hicho.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Juma Yange wakati wa kufunga mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika kwa washiriki kupata nadharia na baadaye vitendo yaliyofanyika kiwanja hicho.
Afande Yange amesema kwa kuwa wafanyakazi wengi hawajui namna ya kujiokoa wakati wa majanga ya moto, hivyo wanafanya mafunzo hayo kuwa endelevu kwa kuyafanya kuwa endelevu, endapo moto utatokea waweze kujiokoa na kuokoa mali.
“Mafunzo haya yana madhumuni ya kuwawez moto kwenye sehemu yake ya kazi, kufahamu vyanzo na vitu vinavyosababisha moto na vifaa vya huduma vya kwanza vya kuzimia moto vilivyopo eneo lake la kazi, hivyo litakuwa endelevu,” amesema.
Kwa upande wake, Bi. Julieth Fonga wa Kampuni ya General Aviation Services inayofanya kazi zake katika jengo la Kwanza la abiria (TBI) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ameomba mafunzo hayo kutolewa mara kwa mara ili kuwaweka tayari kwa janga hilo la moto.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sajini Maria Gulam amesema wananchi wawe makini na moto, ambao unatokana na muunganiko wa kemikali unaofanywa na vitu vitatu kwa uwiano maalum, ambavyo ni joto, hewa safi na kiwashio.
Sajini Gulam amesema wananchi watambue kuwa moto upo katika madaraja manne ambayo ni ‘A’ yenye viwashio vya asili kama majani, kuni, mkaa, karatasi; daraja ‘B’ inaviwashio vya asili ya kimiminika kama mafuta taa, petrol, diseli, mafuta ya kula; huku daraja ‘C’ ni asili ya gesi na ‘D’ inatokana na michemko ya madini na hutokea zaidi kwenyte viwanda vya kutengeneza mabati, mitambo ya vipuri.
Hata hivyo, Sajini Gulam amesema mafunzo haya ya zimamoto na uokoaji yanatolewa kwa taasisi za umma na binafsi kwa gharama nafuu, ili waweze kujua namna ya kujiokoa na kupiga simu namba 114 ya kuomba msaada wa gari la zimamoto.
Mkaguzi Zimamoto Theresia Tengia (kushoto) na Sajini Maria Gulam (kulia) wakionesha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zinazoendesha shughuli zake kwenye Kuiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), moja ya kifaa aina ya blanketi linalosaidia kuzima na kufunika moto endapo utatokea bila kumuathiri kwa kuungua. Sajini Maria Gulam (mbele) akionesha namna ya kutumia mtungi wa kuzimia moto kwa washiriki wa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto kilichopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Bi. Julieth Fonga (kushoto) wa Kampuni ya General Aviation Services iliyopo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akielekezwa na Afisa Usalama wa Zimamoto na Uokoaji, Leonard Chami namna ya kuzima moto kwa kutumia mtungi, wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo kwenye kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha JNIA.
Afisa TEHAMA, Bw. Geofrey Youze akifanya zoezi la kuzima moto katika mafunzo yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Sajini Maria Gulam leo katika mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika katika Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akionesha namba ya kupiga endapo Mwananchi atakuwa amepata tatizo la moto, ili apate msaada wa haraka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni