Wananchi wa Afrika Kusini wamekusanyika
kwenye makanisa, misikiti pamoja na kwenye mahekalu ya ibada hii leo
kumkumbuka na kumuombea aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson
Mandela, ambaye ujumbe wake wa amani na mapatano ulijenga umoja
katika taifa hilo.
Maombi hayo ya kitaifa yanafungua rasmi
maombolezo ya wiki moja kabla ya maziko ya kitaifa ya kiongozi huyo
aliyefanikiwa kuvunja ubaguzi wa makaburu nchini Afrika Kusini wakati
wa zama za ubaguzi, na kujenga taifa lenye kuzingatia usawa na
demokrasia.
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe
Michelle watahudhuria ibada ya kumbukumbu ya Mandela siku ya Jumanne
Jijini Johannesburg, huku idadi kubwa ya viongozi wa dunia
wakitarajiwa kwenda Afrika Kusini kutoa heshima zao za mwisho kwa
shujaa huyo wa vita vya ubaguzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni