Malkia Elizaberth akiwa na Nelson Mandela enzi za uhai wake
Rais wa Marekani Barak Obama akiwa katika sura ya majonzi
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na mkewe Samantha wakiwa na Nelson Mandela wakati wa sherehe ya kumbukumbu yake ya kutimiza miaka 90
Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W.Bush akiwa na Nelson Mandela. Picha hii walipiga mwaka 2001
Uwanja huu wa michezo uliopo jijini Johannesburg uliotumika katika fainali za kombe la Dunia mwaka 2010 ndio utaokutumika kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao Nelson Mandela
Kwaheri Madiba, tabasamu hili tutalikosa milele
Wakati Malkia Elizaberth wa Uingereza akishindwa kuhudhuria shughuli za mazishi za Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela kutokana na kushauriwa kutosafiri safari ndefu,malkia huyo sasa atawakilishwa na Prince Charles.
Zaidi ya viongozi 140 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni watahudhuria maziko hayo jumapili ijayo ya tarehe 15/12/2013 huko Afrika Kusini.
Rais Barak Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama, ataungana na marais waliomtangulia akiwemo George W.Bush na mkewe Laura pamoja na Bill Clinton na mkewe waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton katika mazishi ya shujaa huyo.
Pia Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis na Dalai Lama nao wanatarajiwa kushiriki mazishi hayo akiwemo pia waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na mkewe.
Watu wengine mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria maziko hayo ni pamoja na Bill Gates, Oprah, Naomi Campbell.
Ibada ya mazishi inatazamiwa kuendeshwa na Askofu Desmond Tutu ambaye pia alikuwa rafiki na mtu wa karibu sana na Nelson Mandela.
Endelea kufuatilia kila mara www.rweyunga.blogspot.com kwa taarifa zaidi toka Afrika Kusini hadi siku za maziko ya shujaa huyu NELSON MANDELA " MADIBA "
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni