Kocha wa Manchester United David Moyes
amesisitiza kuwa timu yake bado ipo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa
Ligi Kuu ya Uingereza licha ya kupata kipigo cha pili mfululizo
katika dimba la nyumbani hapo jana.
Newcastle jana ilipata ushindi wa bao
moja bila, ushindi ambao ni wa kwanza kwa klabu hiyo katika dimba la
Old Trafford tangu miaka 41 kupita, na kuifanya Manchester United
kufikisha rekodi ya kufungwa mara tatu nyumbani katika msimu huu.
Wakati huo huo kocha Jose Mourinho
amesema Chelsea ipo katika matatizo baada ya kuongoza kwa bao 1-0, na
baadae kujikuta wakizidiwa kete na kulala kwa mabao 3-2 wakiwa
ugenini dhidi ya Stoke City.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni