Bayern Munich imeichakaza bila ya
hurumu Werder Bremen kwa kuipa kipigo kikali cha mabao 7-0, ikiwa ni
salamu tosha kwa Manchester City ambayo itasafiri wiki ijayo hadi
Ujerumani kucheza nao mchezo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Franck Ribery ndie alikuwa chachu ya
ushindi baada ya kutikisa nyavu mara mbili, na kutengeneza nafasi
nyingine wakati mabingwa hao wakionekana kutoshikika katika ligi hiyo
na kuhakikisha wanalitwa tena taji lao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni