.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 10 Desemba 2013

RAIS KIKWETE AWASILI PRETORIA KUHUDHURIA IBADA KUU (MEMORIAL SERVICE) YA KITAIFA YA MSIBA WA NELSON MANDELA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
                                                                     PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili katika mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria usiku wa leo, Jumatatu, Desemba 9, 2013, kuhudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa (Memorial Service) ya msiba wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee  Nelson R. Mandela kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg.

Rais Kikwete anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21.

Rais Kikwete ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na mkewe Mama Asha, Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana, Katibu wa Mkuu wa CCM.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni