Banda kubwa limeanza kujengwa katika
eneo la uwanja wa nyumba ya Nelson Mandela litakalotumika kwa ajili
ya shughuli ya mazishi yake makubwa kuwahi kufanyika katika historia
ya nchi ya Afrika Kusini.
Maandalizi ya mwisho mwisho yanafanyika
kabla ya viongozi zaidi ya 70 duniani kuja Afrika Kusini wiki hii
kuhudhuria maziko ya mwanasiasa huyo maarufu duniani kwa harakati
zake za kudai haki na kupigania amani.
Taarifa zilizotufikia hivi karibuni
zinasema Rais Raul Castro wa Cuba na Robert Mugabe wa Zimbabwe nao
watakuwemo miongoni mwa wageni kama Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron, Prince Charles pamoja na Rais Barack Obama pamoja na
wengineo wengi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni