Chama cha Watumishi wa Afya nchini
Kenya kimeitisha mgomo wa kitaifa baada ya kushindwa kufikia muafaka
na serikali.
Katibu wa Chama cha Madaktari,
Wafamasia na Madaktari wa Meno, Sultani Matendechere ametangaza kuwa
mgomo huo utaanza usiku wa kuamkia leo katika hospitali zote za umma.
Watumishi hao wa afya wanapinga hatua
ya serikali kuhamishia huduma za afya ikiwemo malipo ya mishahara yao
kuwa chini ya serikali za kaunti.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni