.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Januari 2014

MWANAMKE KENYA ACHINJA MBWA WAWILI NA KULA NYAMA YAO KUKABILIAN NA NJAA

Polisi katika kaunti ya Turkana nchini Kenya wamemuachia huru mwanamke mmoja aliyechinja mbwa wawili na kula nyama zao na familia yake ili kuweza kuishi kutokana na njaa kali iliyopo kwenye kaunti hiyo.

Mwanamke huyo Akai Ekomua alisema kisa cha kuchinja mbwa wake ni ili apate nyama ya kula na familia yake iliyopo kwenye njaa na pia aliwagaiwia majirani zake nao ili wajinusuru na baa la njaa.

Mwanamke huyo aliyefiwa na watoto watatu kutokana na njaa hiyo, amelieleza jeshi la polisi kuwa aliamua kuchinja mbwa hao, kwa kuwa aliogopa kuvunja sheria iwapo angeiba mbuzi kwa majirani zake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni