.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Januari 2014

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MHARIRI ABSALOM KIBANDA NA WENZAKE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda, Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited Theophil Makunga na mwandishi Samson Mwigamba.

Akisoma hukumu hiyo Jijini Dar es Salaam, Hakimu Mkazi Warialwande Lema amesema washtakiwa hao walishtakiwa kwa hisia tu na hisia haziwezi kuwa na mashiko hata zikiwa na nguvu ya aina gani na kuongeza kuwa ushahidi uliowasilishwa dhidi yao ulikuwa dhaifu.

Makunga na wenzake Absalom Kibanda na Samson Mwigamba walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye gazeti la Tanzania Daima yenye maneno yaliyolenga kuwashawishi wasitii viongozi wao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni