Licha ya kuwa kivutio kwa uhusika
wake katika filamu ya 12 Years A Slave, muigizaji filamu Lupita
Nyong'o sasa amekuwa akinyemelewa mno na wabunifu wa mavazi wa Kimataifa ili avae nguo zao kuzitangaza.
Miongoni mwao zimo kampuni kubwa za
mavazi za Uingereza za Stella McCartney na Alexander McQueen, ambazo
zinamuomba Lupita raia wa Kenya kuvaa nguo zao kwenye tuzo za Oscar,
baada ya kuvaa gauni la Dior katika tuzo za BAFTA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni