
Timu ya Bayern Munich huenda ikajikuta matatani mbele ya UEFA baada ya baadhi ya mashabiki wake kuonyesha tambara lenye picha yenye maandishi ya kumdhihaki mchezaji wa Arsenal kuwa ni shoga.
Bango hilo lililoonyeshwa jana usiku katika kipindi cha pili cha mchezo wao wa Klabu Bingwa Ulaya liliandikwa “Gay Gunners” likiwa na picha ya mchoro wa kiungo Mesut Ozil mbele ya mzinga ambao ni nembo ya klabu ya Arsenal.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni