Kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius imeendelea leo huku mtaalam wa uchuguzi wa uhalifu akitoa maelezo kwa vitendo akionyesha namna mwanariadha huyo alipojaribu kuvunja mlango wa choo kwa gongo la kuchezea Kriketi baada ya kumpiga risasi Reeva Steenkamp.
Polisi Johannes Vermeule mwenye cheo Kanali ameiambia mahakama wakati huo Pistorius hakuwa amevalia miguu yake ya bandia kutokana na urefu wa eneo alilokuwa akijaribu kuvunja mlango kuwa chini kiasi
Ushahidi huo ni muhimu kutokana kukinzana na taarifa za Pistorius kuwa alisogelea mlango wa bafu Februari 14 mwaka jana akiwa amevaa miguu yake bandia wakati alipofyatua risasi chooni akidhani kuwa amevamiwa na mtu na kumua mpenzi wake ReevaOscar Pistorius akiwa mahakama hii leo wakati kesi yake ikiendelea kuunguruma


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni