
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wameridhia kuipitisha kanuni za bunge hilo, isipokuwa vifungu namba 37 na 38 ambavyo vinazungumzia utaratibu wa upigaji kura, ambavyo hatma yake itaamuliwa baadae.
Akitoa hoja ya kuridhiwa Kanuni hizo Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof. Costa Mahalu aliwaomba wajumbe wa bunge maalum la Katiba kuridhia kupitishwa kwa kanuni hizo isipokuwa vifungu namba 37 na 38.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Amer Kificho aliwaongoza wajumbe kupigia kura kanuni hizo kwa utaratibu wa kupaza sauti za ndio na sio ambapo waliosema ndio sauti zao zilikuwa nyingi ikilinganishwa na waliosema sio.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni