Kikundi cha al-Shabaab chenye
uhusiano na Al-Qaeda leo kimeapa kuhamishia vita ya Somalia nchini
Kenya, ambapo mmoja wa makamanda wao amesikika akiwataka wapiganaji
wa kundi hilo kuishambulia Kenya.
Akiongea kwenye kituo cha radio cha
Andalus hii leo mmoja wa makamanda wa juu wa al-Shabaab, Fuad Mohamed
Khalaf amesema watahamisha vita Kenya na iwapo watamuua msichana wa
Somalia nao wataua msichana wa Kenya.
Khalifa ambaye alikuwa akiongea
kwenye redio hiyo inayomilikiwa na al-Shabaab amesikika akitoa wito
kwa waislam wa Kenya kupigana na serikali yao, kwa madai kuwa Kenya
imekuwa ikiwauwa ndugu zao na watoto wa Somalia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni