Nchi ya China inatarajia kutuma meli
tano kuwahamisha raia wake kutoka Vietnam kufuatia kuibuka kwa wimbi
la ghasi za kupinga uwepo wa raia wa nchi hiyo huko Vietnam.
Serikali ya China tayari imeshahamisha
zaidi ya raia wake 3,000 kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la
umma.
Meli ya kwanza imeanza safari hii leo,
wakati ambapo raia 16 wa China walioumizwa vibaya wakiondolewa
Vietnam kwa kutumia ndege.
Ghasi hizo za kuwapinga raia wa China
zimepelekea kutokea kwa vifo vya wachina wawili na wengine kadhaa
kujeruhiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni