Viongozi wa Afrika wanaokutana Jijini
Paris wamekubalia kuanzisha vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa
Kiislam la Boko Haram nchin Nigeria.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande
ambaye ndie mwenyeji wa mkutano huo, amesema nchi hizo zimekubaliana
kuchangia taarifa za kiitelenjisia pamoja na kushirikiana kukabiliana
na kundi la Boko Haram.
Mwezi uliopita kundi hilo liliwateka
wanafunzi wasichana 223 kaskazini mashariki mwa Nigeria. Pia
kumeibuka na mashambulio mapya yaliyofanywa na kundi hilo nchini
Nigeria na Cameroon usiku wa kuamkia leo.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni