Kocha Barcelona Gerardo Martino
ataachia ngazi kuinoa klabu hiyo kwa maridhiano ya pande mbili baada
ya kushindwa kuipatia kombe la Ligi ya La Liga.
Barcelona ilikuwa inahitaji ushindi
dhidi ya Atletico Madrid ili kutwaa kombe katika mchezo wao wa mwisho
hapo jana lakini ikajikuta ikitoka sare ya bao 1-1.
Matokeo hayo yanaifanya Barcelona
kumaliza msimu huu bila kutwaa kikombe kikubwa chochote tangu mwaka
2007-2008.
Akiongelea matokeo hayo Kocha Martino,
ameomba msamaha kwa kushindwa kufanya vyema, na amewashukuru
mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwa na imani naye.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni